WHO yaunga mkono kampeni ya dharura ya kutoa chanjo ya polio nchini Malawi baada ya kubainika kwa mgonjwa wa polio
20 February 2026

WHO yaunga mkono kampeni ya dharura ya kutoa chanjo ya polio nchini Malawi baada ya kubainika kwa mgonjwa wa polio

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

About
Takribani watoto milioni 1.3 nchini Malawi wamepatiwa chanjo ya polio katika kampeni maalum ya siku nne, kufuatia kugunduliwa kwa mgonjwa mpya wa polio mwishoni mwa mwezi Januari 2026. Huyu ni mgonjwa wa kwanza kuripotiwa tangu mwaka 2022, wakati virusi vya polio pori vilivyokuwa na uhusiano wa kijenetiki na mlipuko ulioripotiwa nchini Pakistan vilipobainika. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi.