Skip to content
zeno
Create a Station
Explore
Religious
Music
News
Podcasts
Bible
By Genre
By Location
By Language
Download App
Opens in a new window
Toggle Sidebar
zeno
United Nations
Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Daily News
Swahili
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Website
Episodes
Episodes
100
11 September 2026
Katibu Mkuu awaenzi waathirika wa Septemba 11: “Ni shambulio dhidi ya ubinadamu wenyewe”
Miaka 25 baada ya mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11, 2001, yaliyotikisa Marekani na dunia nzima, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amewaenzi karibu watu elfu tatu waliopoteza maisha, manusura na wahudumu wa huduma ya kwanza waliojitolea kuokoa wengine. Kwa wale waliokuwa New York siku hiyo, kumbukumbu ya mashambulizi hayo bado ni ya hofu, mshikamano na athari ambazo...
2 min
11 September 2026
Changamoto ndani ya mafanikio ya mradi wa kuongeza kipato na kulinda mazingira Kwale, nchini Kenya
Nchini Kenya, mradi wa kuboresha mbinu za kipato za wavuvi na kulinda mazingira unaotekelezwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa kupitia Kamisheni ya Masuala ya Uvuvi kwa Ukanda wa Kusini-Magharibi mwa bahari ya Hindi (SWIOFC) umeanza kuleta nuru kwa jamii za wavuvi kwenye kaunti ya Kwale nchini humo. Kwa sasa kiwango cha uvuvi mathalani dagaa kimeongezeka na kuibua changamoto ndani ya mafanikio.
2 min
11 September 2026
Majanga ya tabianchi yavuruga masomo ya watoto milioni 171 duniani - UNICEF
Zaidi ya wanafunzi milioni 171 duniani sawa na mwanafunzi mmoja kati ya kila kumi wa umri wa kusoma shule walikumbwa na usumbufu wa masomo kutokana na majanga ya tabianchi mwaka 2025 kwa mujibu wa uchambuzi mpya uliotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF. Taarifa ya Flora Nducha inafafanua zaidi
3 min
11 September 2026
11 SEPTEMBA 2026
Hii leo tunaangazia miaka 25 baada ya mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11, 2001, elimu na athari za mabadiliko ya tabianchi, na mbinu za kipato za wavuvi na ulinzi wa mazingira nchini Kenya.Miaka 25 baada ya mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11, 2001, yaliyotikisa Marekani na dunia nzima, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amewaenzi karibu watu elfu tatu waliopoteza maisha,...
11 min
10 September 2026
10 SEPTEMBA 2026
Mada kwa kina ambayo leo inamulika jinsi Umoja wa Mataifa ulivyobaini umuhimu wa kujumuisha harakati za kutokomeza mlipuko wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na usaidizi wa chakula kwa wagonjwa, familia zao na wahudumu wa afya. Mwakilishi Mkazi wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP David Stevenson ametanabaisha hayo wakati wa mahojiano yake na Dianne...
9 min
09 September 2026
09 SEPTEMBA 2026
Kikosi cha 12 cha Ulinzi wa Amani kutoka Tanzania kinachohudumu nchini Jamhuri ya Kidemkrasia Congo DRC chini ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda amani nchini DRC, MONUSCO kimefanikiwa kurejesha amani katika kijiji cha Sayo kilichopo katika mji wa Beni. jimboni Kivu KaskaziniTuungane na Private Lazaro Richard Mlyuka aliyetuandalia mada hii kwa kwa kina akieleza juhudi zilizofanyika na...
9 min
08 September 2026
08 SEPTEMBA 2026
Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuleteaShirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO linasema kuwa uvutaji sigara una uwezekano mkubwa wa kufanya iwe vigumu kwa mwanamke au mwanaume kupata mtotolikieleza kuwa wanawake wanaovuta sigara wana hatari kwa juu ya asilimia 40 kupata ugumba ikilinganishwa na wasiovuta sigara. Inakadiriwa kuwa takribani kaya moja...
9 min
04 September 2026
04 SEPTEMBA 2026
JP RWEE ni kifupi cha maneno ya lugha ya Kiingereza ambayo kwa lugha ya Kiswahili ni Mpango wa Pamoja wa Kuharakisha Hatua kuelekea Uwezeshaji wa Kiuchumi wa Wanawake wa Vijijini. Huu ni mpango wa kimataifa unaolenga kuhakikisha upatikanaji wa maisha endelevu na kulinda haki za wanawake wa vijijini katika muktadha wa maendeleo endelevu. Mpango huo unatekelezwa kwa pamoja na mashirika ya Umoja wa...
11 min
03 September 2026
03 SEPTEMBA 2026
Dunia iko katika mbio dhidi ya muda kuzuia ongezeko la joto duniani lisivuke nyuzi joto 1.5 Celsius. Lakini wanasayansi wanaonya kwamba kiwango hicho kinaweza kuvukwa katika miaka michache ijayo. Hali hiyo inajulikana kama “overshoot” kipindi ambacho joto duniani linapanda juu ya nyuzi joto 1.5, kabla ya kushuka tena. Je, kuvuka kiwango hicho kunamaanisha tumeshindwa? Au bado kuna nafasi ya...
9 min
03 September 2026
Kuvuka kiwango cha nyuzi joto 1.5°C: sio sababu ya dunia kukata tamaa
Dunia iko katika mbio dhidi ya muda kuzuia ongezeko la joto duniani lisivuke nyuzi joto 1.5 Celsius. Lakini wanasayansi wanaonya kwamba kiwango hicho kinaweza kuvukwa katika miaka michache ijayo. Hali hiyo inajulikana kama “overshoot” kipindi ambacho joto duniani linapanda juu ya nyuzi joto 1.5, kabla ya kushuka tena. Je, kuvuka kiwango hicho kunamaanisha tumeshindwa? Au bado kuna nafasi ya...
6 min