Watengeneza maudhui kupoteza mapato kutokana na kasi ya maendeleo ya Akili Mnemba
18 February 2026

Watengeneza maudhui kupoteza mapato kutokana na kasi ya maendeleo ya Akili Mnemba

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

About
Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, limesema wabunifu wa maudhui duniani kwa lugha ya kiingereza content creators wanakabiliwa na hatari ya kupoteza hadi asilimia 24 ya mapato yao ifikapo mwaka 2028 kutokana na kasi ya maendeleo ya Akili Mnemba, au AI. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi.