
09 January 2026
UNICEF yaonya uhaba wa fedha wawaweka na watoto hatarini nchini Sudan
Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
About
Leo imetimia siku 1000 tangu kuzuka kwa vita nchini Sudan, vita vinavyohusisha Jeshi la Sudan SAF na Kikosi cha Wanamgambo wa Sudan cha Msaada wa Haraka RSF. Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM limesema mtu mmoja kati ya watatu nchini humo ni mkimbizi ndani ya nchi yake au amekimbilia nje ya nchi huku Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF likieleza mzozo huo ambao umeendelea kusababisha janga kubwa la kibinadamu unawatesa zaidi wanawake na watoto kwani wanabeba mzigo mkubwa wa madhara ya vita. Tuungane na Rashid Malekela kwa taarifa zaidi