Skip to content
Opens in a new window
UNICEF yaimarisha lishe ya watoto kupitia usindikaji wa vyakula Njombe nchini Tanzania
19 October 2026

UNICEF yaimarisha lishe ya watoto kupitia usindikaji wa vyakula Njombe nchini Tanzania

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

About
Nchini Tanzania, katika Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, kwa kushirikiana na Halmashauri ya Ludewa kupitia mradi wa Lishe ya Mwanao, linasaidia jamii kukabiliana na udumavu kwa watoto wenye umri wa chini ya ya miaka mitano. Kupitia mafunzo ya usindikaji wa vyakula vinavyopatikana katika maeneo yao, familia sasa zinaweza kupata vyakula vyenye virutubisho kwa muda mrefu, huku baadhi ya wanawake wakipata fursa za kujiongezea kipato. Cynthia Akhangwa na taarifa zaidi.