UNDP yahimiza usalama kwa wachimbaji wadogo wa madini ya ujenzi Tanzania
22 April 2026

UNDP yahimiza usalama kwa wachimbaji wadogo wa madini ya ujenzi Tanzania

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

About
Shirika la Umoja wa Mataifa  la Mpango wa Maendeleo (UNDP), kwa kushirikiana na Tume ya Madini nchini  Tanzania katikati mwa wiki iliyopita yaani Aprili 16 na 17 wamefanya warsha ya mafunzo mkoani Singida katikati mwa nchi. Mafunzo hayo yamelenga kuimarisha ujuzi wa uchimbaji salama, unaozingatia sheria, na wenye faida kwa wanawake na vijana wanaojihusisha na uchimbaji mdogo wa madini ya ujenzi. Rashid Malekela na taarifa zaidi.