
01 April 2026
Ukandamizaji wa uhuru wa kujieleza huko Mashariki ya Kati - Türk
Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
About
Tangu kuanza kwa mashambulizi ya Marekani na Israeli dhidi ya Iran, ukandamizaji wa nafasi ya kiraia na uhuru wa kujieleza umeongezeka kwa kiasi kikubwa kwenye eneo la Mashariki ya Kati, ukiongeza hali ya hofu iliyokuwepo tayari kutokana na migogoro na misukosuko mingi, ameonya hii leo Kamishna Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, Volker Türk. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.