02 October 2026
“Maisha yanaweza kuwa mabaya kwa sababu ya vita, lakini tunaimba tu… na ninapoimba inanifanya kusahau matatizo yote na kuwa katika wakati huo." - Toussaint Chiza
Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
About
Mwaka huu ni miaka 75 tangu ulipopitishwa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Wakimbizi mwaka 1951 na tangu wakati huo mamilioni ya wakimbizi wamepatiwa hifahi, usalama na maisha yao kuokolewa na kubadilishwa kupitia mpango wa mkataba huo wa kuwapeleka wakimbizi katika nchi ya tatu kuanza upya maisha yao. Miongoni mwa wafaidika wa mpango huo ni mgeni wetu kwenye mada ya leo aliyekimbia vita Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, hadi Uganda na kisha nchini Sweden ambako sasa ni mwanaharakati wa kuchagiza haki za wakimbizi, mwanamuziki na Balozi mwema wa Kitaifa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR. Amezungumza na Flora Nducha wa Idhaa hii kuhusu safari hiyo ya mafanikio.