
22 April 2026
Kilimo endelevu charejesha matumaini ya kujitegemea Kakuma, Neema aibuka kutoka utegemezi hadi uzalishaji
Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
About
Maisha ya wakimbizi katika eneo la Kakuma, kaskazini mwa Kenya, yanaanza kubadilika kwa kasi kupitia miradi ya kilimo na lishe inayowezeshwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo lile la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na la Chakula na Kilimo (FAO). Kwa ushirikiano na Serikali ya Kaunti ya Turkana chini ya ufadhili wa Muungano wa Ulaya (EU) sasa wakimbizi wana uwezo wa kuzalisha chakula chao wenyewe, kuboresha lishe, na kujenga maisha ya kujitegemea. Feissal Kirwa anasimulia.