
28 November 2025
Katibu Mkuu wa UN ameitaka Guinea-Bissau kurejesha utawala wa kikatiba mara moja
Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
About
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, amelaani vikali mapinduzi yanayoendelea nchini Guinea-Bissau akitaka “urejeshwaji wa haraka na usio na masharti wa utawala wa kikatiba” baada ya wanajeshi kutwaa madaraka kufuatia uchaguzi mkuu wa uliofanyika tarehe 23 Novemba. Selina Jerobon na maelezo zaidi.