Skip to content
Opens in a new window
FAO yawezesha wanawake na vijana katika sekta ya mwani Zanzibar
17 August 2026

FAO yawezesha wanawake na vijana katika sekta ya mwani Zanzibar

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

About
Nchini Tanzania hususan visiwani Zanzibar, Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, (FAO) tangu mwaka 2019, kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wanaimarisha sekta ya mwani, kwa kuwekeza katika mafunzo yanayolenga kuongeza uzalishaji, tija na kipato. Miongoni mwa walionufaika zaidi ni vikundi vya wanawake, ambavyo vimejengewa uwezo kuhusu mbinu bora za uzalishaji, uanikaji na uhifadhi wa mwani, pamoja na kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi. Assumpta Massoi anatuletea taarifa inayomhusu mnufaika mmoja wa mafunzo hayo.(Taarifa ya Assumpta Massoi)Jumla ya vikundi 33 vya wanawake vimewezeshwa kwa chanja bora za kuanikia mwani na maturubai maalum ya kuufunika wakati wa mvua.Aidha, wanawake wamejengewa uwezo kuhusu teknolojia ya kilimo mchanganyiko inayowawezesha kulima mwani sambamba na kufuga majongoo bahari.Teknolojia hii inalenga kuongeza tija, kuboresha matumizi ya rasilimali za bahari na kuwawezesha wanawake kupata vyanzo mbalimbali vya kipato.FAO pia imewawezesha vijana kupitia Zanzibar Technology and Business Incubator (ZTBI), kwa kuwapatia mafunzo kuhusu usindikaji, ubunifu na uongezaji thamani wa bidhaa za mwani. Mafunzo hayo yamejikita pia katika uboreshaji wa ubora, upatikanaji wa ithibati na masoko, huku vijana wakipatiwa vifaa vya kuendeleza uzalishaji na ujasiriamali katika sekta ya mwani.