Elimu ya haki za kisheria inapaswa kutumia lugha inayoeleweka na jamii - Wakili Mengo
31 March 2026

Elimu ya haki za kisheria inapaswa kutumia lugha inayoeleweka na jamii - Wakili Mengo

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

About
Wiki iliyopita Kikao cha 70 cha Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani CSW70 kilikunja jamvi baada ya wiki mbili za kujadili mada ya haki, haki za kisheria na kuchukua hatua kuhakikisha haki za wanawake na wasichana zinapatikana. Flora Nducha wa Idhaa hili kandoni mwa kikao hicho alipata fursa ya kuzungumza na Onyonge Mengo kijana mpigania haki za wanawake, mtafiti na wakili kutoka Mahakama Kuu ya Kenya  ambaye pia anafanyakazi na shirika la kimataifa la maendeleo la Hivos ili kufahamu kwa kina nini wanachokifanya kusongesha haki za kisheria za wanawake na wasichana.