Skip to content
Opens in a new window
Baada ya siku 21 bila dalili za ugonjwa, waambata wa mgonjwa wa Ebola Kenya kuondoka kwenye karantini
23 October 2026

Baada ya siku 21 bila dalili za ugonjwa, waambata wa mgonjwa wa Ebola Kenya kuondoka kwenye karantini

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

About
Oktoba 23 2026, ni siku 19 sasa tangu Kenya itangaze kuweko kwa mgonjwa wa Ebola ambaye alifariki dunia tarehe 6 mwezi huu wa Oktoba. Kufuatia tangazo hilo watu waliotambulika kuwa karibu na mgonjwa huyo au waambata waliwekwa karantini kama njia ya kufuatilia iwapo wana maambukizi au la. Kati yao, wanane wamebainika kuwa na maambukizi. Sasa kwa kuwa siku 21 za kuchunguzwa iwapo wengine wana maambukizi au la zinakaribia kutimia, Wizara ya Afya ya Kenya imetangaza kuwa watu hao wataruhusiwa. Je shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, (WHO) nchini Kenya linazungumziaje hatua hii? Assumpta Massoi wa Idhaa hii aliyeko Kenya amezungumza na Mwakilishi wa WHO nchini humo Dkt. Neema Rusibamayila Kimambo.