About
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Hii leo tunaangazia sekta ya afya barani Afrika na kuzungumzia hilo mwenzangu Leah Mushi amezungumza na Mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni Kanda ya Afrika Profesa Mohamed Janabi.
Suala la kwanza kutaka kufangamu kutoka kwake ni je mkutano wa Ngazi ya Juu kuhusu maandalizi dhidi ya majanga ya milipuko ya magonjwa ulifanyika mwishoni mwa wiki hii umefikia azimio walilotaka kukubaliana?
Pia tunakuletea muhtasari wa habari.
• Hii leo viongozi wa nchi 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa wanashiki kwenye Mkutano wa Ngazi ya Juu ukimulika maadhimisho ya miaka 25 na Mpango wa Utekelezaji wa Azimio la Durban la mwaka 2001 ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema anasikitishwa kuona kwamba ubaguzi wa rangi bado unaendelea duniani, na kwamba kitendo hicho kinahatarisha juhudi za kujenga dunia yenye amani, usawa na heshima kwa watu wote. Akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano huo leo kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kando ya Mjadala Mkuu, (UNGA81) Guterres amesema ubaguzi wa rangi bado “unatia sumu” katika jamii, unazidisha pengo la kijamii na kiuchumi, na kuwanyima watu haki na uhuru wao wa msingi.
• Leo ni siku ya mwisho ya Mjadala Mkuu wa Mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, (UNGA81). Miongoni mwa nchi zilizohutubia asubuhi hii ya saa za New York-Marekani ni Mali ambayo imewakilishwa na Waziri wake wa mambo ya nje Abdoulaye Diop ambaye pamoja na mambo mengine ametoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kutokaa kimya mataifa mengine yanapoingilia uhuru w anchi za Afrika akitoa mfano wa Ukraine kuunga mkono makundi ya kigaidi dhidi ya Mali. Amesisitiza hakupaswi kuwa na kitu cha “ugaidi mzuri na ugaidi mbaya.”.
• Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Eritrea, Osman Saleh Mohammed, akihutubia mjadala huo mkuu amezungumza masuala mengi ambayo Umoja wa Mataifa unapaswa kuyashughulikia akitoa mfano wa athari za kile alichokiita sera ya “MAGA” ya Rais wa Marekani Donald Trump ni miongoni mwa matukio yanayohitaji kuangaliwa katika hali ya sasa ya kimataifa. Aidha ametoa wito wa kusitishwa kwa vita vinavyoendelea katika kanda mbali ukiwemo ukanda wa Sahel, Pembe ya Afrika, Mashariki ya Kati na Ukraine.
Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!