About
Hii leo jaridani tunakuletea Mada kwa Kina. Huko jijini Nairobi Kenya kunahitishwa mkutano wa kimataifa unaofahamika kwa jina The Trust Summit 2026 ulioanza tarehe 21 Oktoba ukiwaleta pamoja viongozi wa serikali, taasisi za kimataifa na wadau wengine kutoka Nyanja mbalimbali duniani.
Ili kuuelewa zaidi kuhusu mkutano huu, Cynthia Akhangwa wa Idhaa hii amefanya mazungumzo na Daniel Wanjohi Ndirangu, Mkurugenzi wa Taasisi ya Fedha za Umma ya nchini Kenya walipokutana katika Makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa jijini New York-Marekani.
Daniel anaanza kwa kurejelea masuala yaliyoangaziwa katika Mjadala Mkuu 81 wa Baraza la Kuu la Umoja wa Mataifa na namna yalivyo na uhusiano na mkutano huu unaofanyika jijini Nairobi.
Pia tunakuletea muhtasari wa habari:
• Naanzia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako mgao wa mlo wa moto unaotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, (WFP) kwa wagonjwa wa Ebola ya virusi vya Bundibugyo na wanafamilia umekuwa nguzo ya mwitikio dhidi ya ugonjwa huo ambao sasa umeenea katika majimbo manane tangu utangazwe rasmi mwezi Mei mwaka huu.
• Kwa upande wake, Dkt. Catherine Smallwood ambaye ni Meneja WHO wa ufuatiliaji wa Ebola nchini DRC akizungumza kutokea jimboni Ituri, mesema pamoja na changamoto ya vifo vya Ebola nchini humo, “habari njema ni kwamba tuna manusura 2,600 wa Ebola ambao pia wanaendelea kusajiliwa. Sasa, kupitia kliniki tunazofungua kwa ajili ya manusura hawa, wanaweza kupata huduma za afya, ikiwemo ufuatiliaji na kuendelea kuwepo kwa virusi mwilini, msaada wa kisaikolojia na kijamii, pamoja na usimamizi wa kitabibu wa madhara au matatizo yoyote ya kiafya yanayoendelea kutokana na ugonjwa huo.”
• Na Mwakilishi wa shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO nchini Kenya Dkt. Neema Rusibamayila Kimambo amezungumzia taarifa ya kwamba Wizara ya Afya hapa Kenya inajiandaa kuwaruhusu waambata wa mgonjwa wa Ebola aliyefariki dunia Oktoba 6 mwaka huu baada ya kuweko karantini kwa siku 21 bila dalili zozote za ugonjwa huo wa virusi vya Bundibugyo.
Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!