
About
Hii leo jaridani tunaangazia uchaguzi wa Barham Ahmed Salih wa kuwa Kamishna Mkuu ajaye wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, Tiba asili, na haki za binadamu nchini Sudan. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, amekaribisha hatua ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ya hapo jana kumchagua Rais Mstaafu wa Iraq, Barham Ahmed Salih wa kuwa Kamishna Mkuu ajaye wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, kwa muhula wa miaka mitano ijayo.Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO, linasema tiba asilia na tiba jadidifu zina nafasi muhimu katika mifumo ya afya duniani, hasa katika kinga, huduma za usaidizi wa magonjwa na kuongeza upatikanaji wa huduma za afya kwa jamii. Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Kitengo cha Tiba Asilia, Jadidifu na Jumuishi cha WHO, Dkt. Sung Chol Kim, katika mahojiano maalum kando ya Mkutano wa Kimataifa wa Tiba Asilia unaoendelea huko New Delhi, IndiaUmoja wa Mataifa unaendelea kuonesha wasiwasi mkubwa kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu katika eneo la Darfur, Sudan, ukionya kuwa mashambulizi yanayolenga makundi maalum ya watu yanaweza kuashiria hatari kubwa zaidi ya mauaji ya kimbari.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!