
About
Hii leo jaridani tunaangazia tiba asili, machafuko katika jimbo la Kivu Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC na ubakaji unaotumika kama silaha ya vita nchini humo humo.Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO, linaweka mkazo mpya wa kisayansi katika tiba asili au mitishamba, wakati mawaziri, wanasayansi na viongozi wa jamii za asili kutoka zaidi ya nchi 100 wakikutana mjini New Delhi India kuanzia leo kuangazia mchango wa tiba za asili.Kuongezeka kwa machafuko katika jimbo la Kivu Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kumesababisha watu wengi kuyahama makazi yao ndani na kumbilia kusaka hofadhi nchi Jirani ya Burundi. Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wakimbizi limeeleza mpaka sasa karibu wakimbizi 64,000 tayari wamewasili Burundi, na idadi ikitarajiwa kuongezeka.Ubakaji unaotumika kama silaha ya vita huacha majeraha yasiyofutika ya mwili, akili na ya roho. Katika ushuhuda huu wenye nguvu, manusura mmoja kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambaye sasa anaishi kama mkimbizi nchini Burundi, anasimulia safari yake ya maumivu baada ya kunusurika ukatili wa kingono uliomsababishia majeraha makubwa ya mwili, ikiwemo fistula, pamoja na makovu ya kina ya kihisia.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!