About
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoangazia silaha za vita zinazojiendesha zenyewe, pamoja na muhtasari wa habari za masuala ya amani na haki za kibinadamu kwa wakimbizi.
• Huko Manila, Ufilipino Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, amehutubia mkutano wa 16 wa pamoja wa nchi za Jumuiya ya Kusini – Mashariki mwa Asia na Umoja wa Mataifa na kutaka mageuzi ya taasisi za kimataifa ili kutoa nafasi na uwakilishi unaostahili kwa mataifa yanayoinukia kiuchumi na kisiasa, akisema mfumo wa sasa hauakisi hali halisi ya dunia inayozidi kuwa na vituo vingi vya mamlaka.
• Kitendo cha kupunguzwa kwa kiasi kikubwa kwa ufadhili wa misaada kinawaweka wakimbizi, hususan watoto, katika hatari kubwa ya kusafirishwa kinyume cha sheria, kutumikishwa au u kufanyiwa ukatili, huku mifumo ya ulinzi inayowalinda ikiendelea kudhoofika. Taarifa hizo ni kwa mujibu wa tafiti mbili mpya za Ethiopia na Bangladesh zilizozinduliwa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) kwa ushirikiano na Chuo cha Nuffield cha Chuo Kikuu cha Oxford nchini Uingereza.
• Na Mkutano wa Saba wa Mapitio wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Kupiga Marufuku au Udhibiti wa Baadhi ya Silaha za Kawaida (CCW), umeanza hii leo huko Geneva, Uswisi ambapo ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ametoa wito mahsusi kwa wajumbe wa mkutano huo unaomalizika Novemba 20 akisema, “hasa, ninawasihi muanze kuelekea katika mazungumzo ya kujadili na kuandaa Mkataba wenye nguvu kisheria utakaodhibiti mifumo ya silaha zinazojiendesha zenyewe ikijumuisha kuweka makatazo na vikwazo vilivyo wazi. Vipengele vilivyobainishwa na Kundi la Wataalamu wa Serikali kuhusu suala hili vinatoa msingi imara wa kuendeleza juhudi hizi.”
Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!