About
Hii leo jaridani tunaangazia uhakika wa chakula nchini DRC, kilmo na mbegu bora nchin Zimbabwe, na biashara ndogondogo na ufugaji kuku kwa wanawake wenye ulemavu nchini Kenya.
• Kwa mujibu wa Mfumo wa Umoja wa Umoja wa Mataifa wa tathimini ya viwango vya uhakika wa chakula IPC, hali ya uhaba mkubwa wa chakula inatarajiwa kuwa mbaya zaidi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), watu milioni 30.3 wakitarajiwa kukabiliwa na uhaba wa chakula wa viwango vya janga au hali mbaya zaidi kati ya mwezi Januari na Juni 2027. Anold Kayanda ameifuatilia ripoti hii na anaeleza kwa kina
• Nchini Kenya, Pikoti Chepkemoi, mwanamke mwenye ulemavu wa miguu kutoka Kaunti ya Pokot Magharibi, ameweza kujikwamua kiuchumi licha ya kuwa na changamoto za ulemavu huo tangu utotoni. Kupitia mafunzo ya ufugaji wa kuku na biashara ndogondogo yanayoambatana na ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya Wanawake, UN Women ndoto yake imetia.
• Nchini Zimbabwe, ambako ukame unaathiri uzalishaji wa chakula, Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO, linawasaidia wakulima kutumia mbinu za kuhifadhi maji, kuboresha ufugaji na kutunza mbegu za asili. Kupitia ushirikiano na serikali ya nchi hiyo kuanzia mwaka 2022 hadi mwaka huu 2026, wakulima wamepata mbinu za kuimarisha uzalishaji licha ya changamoto za mabadiliko ya tabianchi.
Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!