
About
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoangazia simulizi za waahirika wa Kimbunga Melissaikiwa ni wiki ya pili sasa baada ya kupiga magharibi mwa Jamaica, na kuacha zahma kubwa kwa wakaazi. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na jifunze Kiswahili.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akieleza kuwa na wasiwasi mkubwa kutokana na ripoti za ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na mauaji ya halaiki mjini El Fasher, pamoja na kuongezeka kwa mapigano katika maeneo ya Kordofan nchini Sudan. Guterres amesema “Mtiririko wa silaha na wapiganaji kutoka nje lazima ukatwe. Misaada ya kibinadamu lazima iweze kuwafikia haraka raia wanaohitaji, na mapigano lazima yakome,”.Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jumatano limemchagua Phoebe Okowa kutoka Kenya kuwa Jaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), baada ya duruu nne za upigaji kura. Upigaji kura huo ulifanyika kwa wakati mmoja na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, lakini kwa utaratibu tofauti, kama inavyotakiwa na Katiba ya Mahakama hiyo ya Haki. Bi. Okowa amechaguliwa kwa wingi wa kura ambapo alipata kura 8 katika Baraza la Usalama na kura 106 katika Baraza Kuu.Kumekuwa na ongezeko la uraibu wa nikotini na bidhaa nyingine zinazozalishwa kwa kutumia tumbaku duniani hususani miongoni mwa vijana na tena wengi hivi sasa wanatumia sigara za kielektroniki, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani WHO. Tarehe 17 mpaka 21 Novemba utafanyika mkutano mkubwa kujadili namna serikali, mashirika ya kimataifa na asasi za kiraia zitakavyoweza kusaidia kupambana na janga la tumbaku duniani, linalosababisha vifo zaidi ya milioni saba kila mwaka.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo, mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua maana za neno "KASIMU"Mwenyeji wako ni Sabrina Said Moshi, karibu!