About
Leo Novemba 12 mwaka 2026, serikali ya Kenya inaanza kuhesabu siku 42 za kufuatilia iwapo kutaibuka tena maambukizi ya Ebola. Hii ni baada ya mgonjwa wa mwisho wa Ebola aliyekuwa anapatiwa matibabu kupona. Yeye ni miongoni mwa wagonjwa 9 walioambukizwa Ebola ya Bundibugyo tangu iripotiwe nchini humo Oktoba 5 baada ya mgonjwa wa Ebola kuingia Kenya kutokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) kupitia Uganda. Wagonjwa wawili walifariki dunia na 7 wamepona. Wengi hujiuliza wametibiwa na nini? Assumpta Massoi amezungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Afya ya Umma nchini Kenya ambaye anaanza kwa kujitambulisha.