
About
Hii leo jaridani tunaangazia wito wa kuimarishwa kwa mshikamano wa kimataifa na uwekezaji endelevu kwa wakimbizi nchini Kenya, usugu wa Viuaji- Vyasumu au AMR na utekelezaji wa mradi wa kusambaza nishati ya umeme na vifaa vya nishati nchini Chad.Katika ziara yake ya kwanza rasmi iliyofanyika nchini Kenya kama Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Wakimbizi, Barham Salih ametoa wito wa kuimarishwa kwa mshikamano wa kimataifa na uwekezaji endelevu ili kuwasaidia wakimbizi kujenga upya maisha yao, akionya kuwa upungufu mkubwa wa ufadhili unatishia kurudisha nyuma mafanikio yaliyopatikana kwa juhudi kubwa katika ulinzi na kujitegemea kwa wakimbizi.Shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani linaendelea na juhudi za kupambana na changamoto ya usugu wa Viuaji- Vyasumu au AMR na sasa imetoa miongozo na taratibu za kuhakikisha kuna matumizi sahihi ya dawa na wahudumu wa sekta ya afya katika nchi wanachama wanaendelea kuwapatia mafunzo ili kuzitumia kwa usahihi na kwa uwajibikaji.Nchini Chad, utekelezaji wa mradi wa kusambaza nishati ya umeme PAAET umefanikisha vifaa 145,000 vya nishati ya sola kusambazwa kwa gharama nafuu kwa kaya zilizoko majimbo 23 ya taifa hilo na sasa maisha yamekuwa bora.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!