11 SEPTEMBA 2025
About
Katika Jarida la Habari za Umoja wa Mataifa leo Flora Nducha anakuletea-Utapiamlo kwa watoto katika Ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel umefikia kiwango cha kutisha, huku takwimu mpya zikionesha ongezeko kubwa mwezi Agosti kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa-Umoja wa Mataifa umeanzisha mradi mpya wa miaka mitatu wenye lengo la kusaidia nchi za Afrika Mashariki kukabiliana na matumizi ya kigaidi ya vilipuzi. Kupitia mradi huu, Kenya, Somalia na Uganda zitasaidiwa-Hali nchini Haiti inaendelea kuzorota, sehemu kubwa ya nchi inadhibitiwa na magenge yenye silaha, nusu ya idadi ya watu wanakabiliwa na upungufu wa chakula, na idadi ya watu waliofurushwa  imefikia kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa amesema Tom Fletshe mkuu wa OCHA-Mada kwa kina inatupeleka Uganda watumiaji wa Ziwa Albert wafunguka kuhusu changamoto za uvuvi haramu na faida za ziwa hilo-Na katika jifunze KIswahili leo mtaalam wetu Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "UKWASI!