Skip to content
Opens in a new window
11 NOVEMBA 2026
About
Hii leo jaridani tunaangazia juhudu za kukabiliana na mabadliko ya tabianchi, na mazishi salama ya miili ya waathirika wa Ebola nchini DRC.

• Maendeleo makubwa yaliyopatikana katika matumizi ya nishati safi duniani yanaonesha kuwa mabadiliko ya haraka kuelekea uchumi usiotegemea nishati za kisukuku yanawezekana, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, hii leo huko Antalya Uturuki hii leo wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Viongozi unaofanyika kwenye Mkutano wa 31 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP31
• Tunasalia huko huko Antalya Uturuki kwenye COP31 ambako Sara Pima kutoka Tanzania. Yeye ni Mjumbe wa Kamati ya Mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi akiwakilisha Afrika, lakini pia yuko kwenye majadiliano kuhusu masuala ya jinsia na kujengea uwezo. Hapa anazungumzia kile wanachopatia kipaumbele katika mkutano huo.
• Katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, mazishi salama na yenye heshima yanaendelea kuwa silaha muhimu katika vita dhidi ya Ebola. Wizara ya Afya ya DRC kwa msaada wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni, WHO, na wadau wake, inashirikisha jamii moja kwa moja katika mazishi hayo ili kulinda familia huku mila zikiheshimiwa.
Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!