Skip to content
Opens in a new window
10 SEPTEMBA 2026
About
Mada kwa kina ambayo leo inamulika jinsi Umoja wa Mataifa ulivyobaini umuhimu wa kujumuisha harakati za kutokomeza mlipuko wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na usaidizi wa chakula kwa wagonjwa, familia zao na wahudumu wa afya.  Mwakilishi Mkazi wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP David Stevenson ametanabaisha hayo wakati wa mahojiano yake na Dianne Penn wa Idhaa ya Kiingereza ya Umoja wa Mataifa, mahojiano ambayo yamechakatwa na Assumpta Massoi wa Idhaa hili ya Kiswahili na   kupatikana mada hii. Takwimu zinaonesha tangu kutangazwa rasmi kwa mlipuko huo tarehe 15  mwezi Mei mwaka huu maambukizi ni zaidi ya watu 6,686 huku waliofariki dunia ni 3,226.