About
Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuleteaShirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO linasema kuwa uvutaji sigara una uwezekano mkubwa wa kufanya iwe vigumu kwa mwanamke au mwanaume kupata mtotolikieleza kuwa wanawake wanaovuta sigara wana hatari kwa juu ya asilimia 40 kupata ugumba ikilinganishwa na wasiovuta sigara. Inakadiriwa kuwa takribani kaya moja kati ya kila kaya 4 huko Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli, inaongozwa na mwanamke, ikiwa ni maradufu ya kiwango kilichokuwepo kabla ya kuanza kwa vita vya sasa mwezi Oktoba mwaka 2023 ambapo kaya moja kati ya kila kaya 9 ilikuwa ikiongozwa na mwanamke.Ujumbe kutoka Tanzania Bara na Zanzibar uliokwenda Kenya kujifunza jinsi ya kuboresha mifumo ya hifadhi ya jamii hususan malipo ya fedha taslimu kwa kaya maskini, umelezea wanachoondoka nacho kupitia ziara hiyo iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP, Kenya.Na katika mada kwa kina leo Shirika la Umoja wa Mataifa la Mitaji UNCDF linaendesha Mradi wa Pamoja wa Takwimu kwa ajili ya Mageuzi ya Kidijitali kwenye kilimo huko nchini Tanzania