Skip to content
Opens in a new window
04 SEPTEMBA 2026
About
JP RWEE ni kifupi cha maneno ya lugha ya Kiingereza ambayo kwa lugha ya Kiswahili ni Mpango wa Pamoja wa Kuharakisha Hatua kuelekea Uwezeshaji wa Kiuchumi wa Wanawake wa Vijijini. Huu ni mpango wa kimataifa unaolenga kuhakikisha upatikanaji wa maisha endelevu na kulinda haki za wanawake wa vijijini katika muktadha wa maendeleo endelevu. Mpango huo unatekelezwa kwa pamoja na mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la chakula na kilimo, FAO, Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo, IFAD, la masuala ya wanawake, UN Women na la Mpango wa Chakula Duniani, WFP katika nchi za Ethiopia, Guatemala, Kyrgyzstan, Liberia, Nepal, Niger, visiwa vya Pasifiki, Rwanda, Tanzania na Tunisia. Hivi karibuni tuliangazia Rwanda. Leo Anold Kayanda anatupeleka nchini Tanzania.