
About
Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe wa Katibu Mkuu kuhusu siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu, simulizi ya Mwalimu mwenye ulemavu wa kuona na huduma za afya ya uzazi kwa wasichana vigori nchini Kenya.Umoja wa Mataifa leo Desemba 3 unaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu kwa ujumbe mzito kutoka kwa Katibu Mkuu António Guterres ujumbe unaotaka jamii ziwe si tu zinazoweza kufikiwa na watuwenye ulemavu, bali pia zenye ujumuishi wa kweli.Ili kuyajadili baadhi ya masuala aliyoyagusia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, basi Diana Katabarwa wa redio washirika wetu Uhai FM amezungumza na Mwalimu mwenye ulemavu wa kuona, Bahati Sanga, Katibu wa Chama Cha Wasioona, Mkoa wa Tabora.Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi UNFPA kupitia ufadhili kutoka kwa asasi ya Adolescent Sexual and #ReproductiveHealth Development Impact Bond, limewezesha wasichana nchini Kenya kupata huduma za uzazi wa mpango bila malipo, taarifa muhimu, na kufanya maamuzi sahihi na hivyo kulinda afya zao na kuboresha mustakabali wao.Mwenyeji wako ni Sabrina Moshi, karibu!