About
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Miongoni mwa mikutano iliyochukua nafasi kubwa wakati wa Mjadala Mkuu wa ngazi ya juu wa Kikao cha 81 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa , UNGA81 ni kuhusu Akili Mnembaa u AI.
Pamoja na changamoto zake lakini AI inauweza mkubwa wa kusaidia jamii kutatua changamoto na hata kuondoa taarifa potofu. Waandishi wa habari hawakuachwa nyuma nao walikuwa na mikutano kadhaa kujadili namna watakavyotumia taalum yao kuisaidi jamii. Mwenzangu Leah Mushi amezungumza na Rais wa wahariri wa habari barani Afrika Churchill Otieno aliyehudhuria mikutano kuhusu ubora wa habari pamoja na akili mnemba AI kwa tasnia ya habari. Kwanza anaanza kwa kueleza kubwa lililozungumzwa kwenye mikutano hiyo?
Pia tunakuletea muhtasari wa habari.
• Usiku wa kuamkia jana Jumatano kituo cha kutibu Ebola kwenye kituo cha mpito cha kuhifadhi wakimbizi huko Kigonze, karibu na mji wa Bunia jimboni Ituri, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC), kilichomwa moto, wakati huu ambapo kimesalia kitupu kutokana na wakimbizi kukimbia mashambulio ya mara kwa mara kutoka makundi yaliyojihami..
• Leo ikiwa ni siku ya wazee duniani wakati huu ikielezwa kwamba kila mtu ni mzee mtarajiwa, na ujumbe wa mwaka huu ukiwa “Enzi ya Maisha Marefu: Kufikiria Upya Mifumo kwa Maisha Marefu,” Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, amesema ongezeko la watu wanaoishi muda mrefu linahitaji serikali na taasisi kubadili mifumo ya kijamii na kiuchumi ili kukidhi mahitaji yao. Guterres amesema maisha marefu yatakuwa ni mafanikio makubwa kwa jamii pale tu yanapowezeshwa na maendeleo ya huduma za afya na mifumo ya ulinzi wa kijamii.
• Na leo pia ni siku ya kahawa duniani, ikiwa ni maadhimisho ya kwanza tangu yapitishwe na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka huu. Lengo ni kuangazia zao hilo ambalo sio tu kiburudisho bali pia mbinu ya kujipatia kipato kwa kaya zipatato milioni 25 kwenye nchi zinazoendelea. Brazili, Viet Nam, Colombia zinaongoza kwa uzalishaji wa kahawa, ilhali Marekani na Muungano wa Ulaya zinaongoza kwa kuagiza na kunywa kahawa.”
Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!