
About
Hii leo jaridani tunaangazia ukandamizaji wa nafasi ya kiraia na uhuru wa kujielez tangu mashambulizi ya Marekani na Israeli dhidi ya Iran, mabomu ya kutegwa ardhini na ujumbe wa watetezi wa haki za wanawake na wasichana kutoka Kenya.Tangu kuanza kwa mashambulizi ya Marekani na Israeli dhidi ya Iran, ukandamizaji wa nafasi ya kiraia na uhuru wa kujieleza umeongezeka kwa kiasi kikubwa kwenye eneo la Mashariki ya Kati, ukiongeza hali ya hofu iliyokuwepo tayari kutokana na migogoro na misukosuko mingi, ameonya hii leo Kamishna Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, Volker Türk.Tarehe 4 mwezi Aprili mwaka huu ni siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu mabomu ya kutegwa ardhini ambayo yamekuwa ‘mwiba’ kwa wananchi walioko maeneo siyo tu ya vita hivi sasa bali pia yale ambamo mapigano yamemalizika lakini masalia ya mabomu yanaendelea kutesa wananchi. Nchini Sudan mwanamke mmoja anatekeleza kwa vitendo maudhui ya siku hii mwaka huu ambayo ni Wekeza kwenye amani, wekeza kwenye hatua dhidi ya mabomu ya kutegwa ardhini.Kutoka nchini Kenya, kijana aliyeshiriki mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW70 amezungumzia jinsi vikao kama hivyo vimekuwa fursa kwa watetezi wa haki za wanawake na wasichana kuwasilisha changamoto kutoka maeneo yao na kusaka suluhu kwa pamoja na washiriki wenzao.Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!