THE LORD GOD / MUNGU BWANA .
16 June 2024

THE LORD GOD / MUNGU BWANA .

NENO
About

IBADA YA JUMAPILI

SOMO: BWANA MUNGU

MAHALI: LIFE IN CHRIST MINISTRIES(ZOE),TABATA KIFURU

MNENAJI: PROPHET SIMON CHARISMA

TAREHE: 16/06/2024

Yeremia 32:26-27

BWANA MUNGU ni mmoja siyo wawili. Mungu alijitambulisha Kwa Nabii Yeremia kuwa yeye ni BWANA na MUNGU pia. Huwezi ukamtenga Mungu na Bwana maana ni mmoja. Ikiwa unaamini kuwa kuna Bwana Mungu lazima uamini kuwa hakuna jambo lolote gumu asiloliweza.

Luka 4:6-12

Ikiwa unafunga lazima kufunga kwako kuongozwe na Roho Mtakatifu. Wakati ibilisi anataka Yesu amsujudie , Yesu alimwambia imeandikwa msujudie BWANA MUNGU wako na umwabudu yeye pekee yake. Akimanisha kuwa Yesu Kristo ndiye BWANA MUNGU hivo anapaswa kuabudiwa na kusujudiwa yeye pekee yake.

Pia Yesu Kristo alimjibu shetani kuwa usimjaribu BWANA MUNGU wako. Yesu Kristo ndiye Bwana Mungu. Yesu Kristo ndiye Mungu, ukimuona Yesu umemuona Mungu.

Yohana 20:26-29

Baada ya Tomaso kuweka mkono wake ndani ya ubavu wa Yesu Kristo na kuona sehemu ambapo mkuki ulichoma ubavu wa Yesu , Tomaso alimwambia Yesu, Bwana wangu na Mungu wangu. Akimanisha kuwa Yesu ni Bwana wake na Mungu wake. Yesu Kristo anataka tuamini kwanza kabla ya kuona muujiza katika ulimwengu wa damu na nyama.

2 Petro1:1-2

Kitendo Cha sisi kuzaliwa mara ya pili,tumepokea Imani yenye thamani.Yesu Kristo ndiye Mungu wetu.Huwezi kumtenga Yesu Kristo na Mungu.Maana Yesu ndiye Mungu.

Tito 2:13-14

Kristo Yesu ni Mungu Mkuu na Mwokozi wetu .

Yuda 1:24-25

Kama Wana wa Mungu hatuwezi kujikwaa maana Yesu Kristo ambaye ni Mungu Mkuu pekee yake anatulinda

Warumi 10:9-13

Ukimkiri Yesu Kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana na kuamini moyoni mwako utaokoka.Yesu kama Mungu aliutoa uhai wake na yeye mwenyewe aliutwaa uhai wake.

Nb.Yesu Kristo ndiye Bwana Mungu na kama unaamini hivyo lazima uamini kuwa kwake hakuna lisilowezekana.

Unaweza kufuatilia ibada hii kupitia YouTube Chanel ya mtu wa Mungu kupitia link... https://www.youtube.com/watch?v=3CtEL9vNGwU

Pia unaweza kuwasiliana nasi kupitia namba 0682-599376/0718-646364 Kwa Maombi,ushauri na maelekezo namna ya kufika katika nyumba ya Mungu.