Uchaguzi mkuu Tanzania: Waangalizi wasema haukuzingatia vigezo vya demokrasia
11 November 2025

Uchaguzi mkuu Tanzania: Waangalizi wasema haukuzingatia vigezo vya demokrasia

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

About

Katika makala yetu leo tunaangazia pakubwa Uchaguzi Mkuu nchini Tanzania ambapo Rais Samia Suluhu aliapishwa siku ya Jumatatu kuongoza muhula wa pili, hata hivyo ni uchaguzi ambao ulikumbwa na utata huku waangalizi kutoka jumuiya ya Afrika kusini SADC na wale wa umoja wa Afrika AU wakisema haukuzingatia vigezo vya demokrasia.

Tunaangazia pia taarifa ya Rais Paul Biya, wa Cameroon kuapishwa Alhamisi iliyopita kuongoza nchi hiyo kwa muhula wa nane, huku upinzani ukiitisha maandamano kupinga matokeo yaliyompa Biya ushindi. Lakini pia tutaangazia kongamano la kimataifa la mazingira, COP30 ambalo linafanyika huko Belem, nchini Brazil, kati ya Novemba 10 na 21.