
03 August 2026
El Niño: Wataalam waonya kuhusu mvua kubwa, mafuriko na joto la kali
Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
About
Hali ya hewa ya El Niño inaendelea kuimarika kwa kasi na inatarajiwa kutawala katika kipindi cha kuanzia mwezi Agosti hadi Oktoba mwaka wa 2026, hali itakayoongeza uwezekano wa viwango vya joto kuzidi wastani katika maeneo mengi ya dunia na kusababisha mabadiliko makubwa katika mifumo ya mvua.
Mashirika ya hali ya hewa likiwemo lile la dunia WMO na KMD nchini Kenya, yameongeza utaratibu, huduma za taarifa za hali ya hewa na usaidizi wa tahadhari za mapema ili kusaidia serikali, mashirika ya kibinadamu, sekta zinazozingatia hali ya hewa kama vile kilimo na afya, na jamii zilizo katika mazingira magumu kujiandaa kwa athari zinazoweza kutokea.
Tumezungumza na wataalam, bofya hapo kusikiliza.