11 November 2026
Ajenda ya Nishati Safi na Vitendo Badala ya Maneno Zatawala Mazungumzo ya COP31 Uturuki
Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
About
Katika mkutano wa tabia nchi mwaka huu COP31, jijini Antalya, Uturuki, wadau mbalimbali wamesisitiza dunia kuondoka katika kutoa ahadi na kuanza kuleta matokeo ya haraka na yenye tija.
Sayari imekuwa ikikabiliwa na changamoto kubwa za mabadiliko ya tabianchi, mkutano wa mwaka huu unalenga zaidi kuharakisha mabadiliko ya nishati safi na kusukuma vitendo madhubuti vya kimataifa.
Nchi zimesisitiza kuwa muda wa mijadala umekwisha na ni muda sasa wa utekelezaji wa vitendo.
Nimefanya uchambuzi na Cherop Soy kutoka shirika la Enzi Ijayo, akizungumzia masuala ya nishati safi kama vile matumizi ya magari ya umeme.