About
Zohali ndiyo sayari inayojulikana zaidi kwa pete zake za ajabu. Lakini je, uzuri wake ndio siri yake kubwa zaidi?Katika documentary hii ya Afrika Imara, tunachunguza ukweli wa kushangaza kuhusu Zohali. Utajifunza jinsi pete zake zilivyoundwa, kwa nini huenda zikatoweka siku moja, siri ya dhoruba yenye umbo la hexagon, na miezi yake ya ajabu kama Titan na Enceladus ambayo imekuwa miongoni mwa maeneo muhimu zaidi katika utafutaji wa maisha nje ya Dunia.