zeno
Home
Explore
Religious
Music
News
Podcasts
Bible
By Genre
By Location
By Language
Download App
Log in
Sign up
Toggle Sidebar
zeno
United Nations
Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Daily News
Swahili
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Website
Episodes
100
13 January 2026
Jifunze Kiswahili: Maana za neno "MAHULUCHI"
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo, Mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana za neno "MAHULUCHI"
1 min
13 January 2026
13 JANUARI 2026
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika mwaka mpya 2026 kwa wakazi wa Ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel ambao wanaendelea kukabiliwa na hali ngumu ya maisha katika kambi za wakimbizi na katika makazi ambayo ni magofu na vifusi vya nyumba zilizoharibiwa wakati wa vita baina ya Jeshi la Israel na Wanamgambo wa Hamas.Shirika la Umoja wa Mataifa la...
9 min
12 January 2026
Mkuu wa UNHCR ahimiza mshikamano na suluhu zaidi kwa wakimbizi Kenya
Katika ziara yake ya kwanza rasmi iliyofanyika nchini Kenya kama Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Wakimbizi, Barham Salih ametoa wito wa kuimarishwa kwa mshikamano wa kimataifa na uwekezaji endelevu ili kuwasaidia wakimbizi kujenga upya maisha yao, akionya kuwa upungufu mkubwa wa ufadhili unatishia kurudisha nyuma mafanikio yaliyopatikana kwa juhudi kubwa katika ulinzi na kujitegemea kwa...
3 min
12 January 2026
Nishati ya sola yaleta matumaini mapya kwa raia nchini Chad
Nchini Chad, utekelezaji wa mradi wa kusambaza nishati ya umeme PAAET umefanikisha vifaa 145,000 vya nishati ya sola kusambazwa kwa gharama nafuu kwa kaya zilizoko majimbo 23 ya taifa hilo na sasa maisha yamekuwa bora.
2 min
12 January 2026
12 JANUARI 2026
Hii leo jaridani tunaangazia wito wa kuimarishwa kwa mshikamano wa kimataifa na uwekezaji endelevu kwa wakimbizi nchini Kenya, usugu wa Viuaji- Vyasumu au AMR na utekelezaji wa mradi wa kusambaza nishati ya umeme na vifaa vya nishati nchini Chad.Katika ziara yake ya kwanza rasmi iliyofanyika nchini Kenya kama Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Wakimbizi, Barham Salih ametoa wito wa kuimarishwa...
9 min
12 January 2026
WHO na juhudi za kupambana na usugu wa Viuajijasumu
Shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani linaendelea na juhudi za kupambana na changamoto ya usugu wa Viuaji- Vyasumu au AMR na sasa imetoa miongozo na taratibu za kuhakikisha kuna matumizi sahihi ya dawa na wahudumu wa sekta ya afya katika nchi wanachama wanaendelea kuwapatia mafunzo ili kuzitumia kwa usahihi na kwa uwajibikaji. Tupate tarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi
2 min
09 January 2026
UNICEF yaonya uhaba wa fedha wawaweka na watoto hatarini nchini Sudan
Leo imetimia siku 1000 tangu kuzuka kwa vita nchini Sudan, vita vinavyohusisha Jeshi la Sudan SAF na Kikosi cha Wanamgambo wa Sudan cha Msaada wa Haraka RSF. Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM limesema mtu mmoja kati ya watatu nchini humo ni mkimbizi ndani ya nchi yake au amekimbilia nje ya nchi huku Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF likieleza mzozo huo ambao...
3 min
09 January 2026
Ripoti ya UN yabainisha sintofahamu wanayokumbana nayo waganda kuelekea uchaguzi mkuu
Ikiwa zimebakia siku 6 kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini Uganda, hii leo Umoja wa Mataifa imetoa ripoti inayobainisha kuwa uchaguzi huo utafanyika katika mazingira yaliyogubikwa na ukandamizaji, vitisho dhidi ya wapinzani wa kisiasa, watetezi wa haki za binadamu, na waandishi wa habari. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.
2 min
09 January 2026
09 JANUARI 2026
Hii leo jaridani tunaangazia uchaguzi mkuu nchini Uganda, elimu kwa watoto nchini Sudan leo ikitimia siku 1000 tangu kuzuka kwa vita nchini humo, na juhudi za wanawake za kuhifadhi misitu huko Narok nchini Kenya.Ikiwa zimebakia siku 6 kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini Uganda, hii leo Umoja wa Mataifa imetoa ripoti inayobainisha kuwa uchaguzi huo utafanyika katika mazingira yaliyogubikwa...
11 min
09 January 2026
UNDP Kenya yaunga mkono wanawake wa jamii ya asili Narok katika uhifadhi wa misitu
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, (UNDP), nchini Kenya, kupitia mradi wa kuhimili tabianchi au Climate Promise Guarantee, limewawezesha wanawake wa jamii ya asili katika Kaunti ya Narok, nchini humo kuongoza juhudi za uhifadhi wa misitu huku wakilinda urithi wao wa kitamaduni na kuboresha maisha ya familia zao. Sheilah jepnge’tich na taarifa zaidi.
3 min