About
Wikendi iliyopita, Tanzania ilizundua rasmi Mradi wa Umeme wa Maji wa bwawa la Julius Nyerere, lenye uwezo wa kuzalisha megawati 2,115. Mradi huu, uliogharimu takribani shilingi trilioni 7.45 za Tanzania sawa na karibu dola za Marekani bilioni 2.9, unaongeza kwa kiasi kikubwa uwezo wa Tanzania kuzalisha umeme.
Katika Makala ya Gurudumu la uchumi wiki hii, tunajiuluza Je, megawati hizi zitageuka kuwa uzalishaji, ajira, biashara na ukuaji wa uchumi?