Changu Chako Chako Changu: Zanzibar yavunja rekodi ya utamaduni wa kufturisha
12 March 2026

Changu Chako Chako Changu: Zanzibar yavunja rekodi ya utamaduni wa kufturisha

Changu Chako, Chako Changu

About

Karibu katika Makala yetu ya leo Changu Chako Chako Changu, makala ambayo hukuletea Historia ya mambo mbalimbali utamaduni, le parler francophone na Muziki, ambapo leo nakupeleka huko Visiwani Zanzibar kuzungumzia utamaduni wa kufturisha ambapo JMarch 7 umati wa watu ulijitokeza kuhudhuria Iftar ilioandaliwa kwa mara ya kwanza kwenye ngazi ya Kitaifa. Tutahitimisha na Muziki kutoka visiwani Zanzibar. Ali Bilali ninakukaribisha karibu, ama bienvenue.

Utamaduni wa kufturisha ni zoezi la kijamii na kidini katika Uislamu ambapo waumini wenye uwezo hutoa chakula na vinywaji kwa waliofunga (wengine) wakati wa kuvunja saumu (futari) katika mwezi mtukufu wa Ramadhani. Inalenga kuimarisha umoja, kusaidia wenye uhitaji, kueneza upendo, na kupata thawabu kwa kushirikiana na wengine. 

Utamaduni huu hufanyika kila mwaka visiwani Zanzibar, kwenye ngazi mbalimbali, kijamii, kitaasisi, lakini mwaka huu imeandaliwa Iftar ya Kitaifa, kwa mujibu wa ofisi ya mtakwimu mkuu wa serikali Zanzibar watu 27345 kati yao wanaume ni elfu 18 771 sawa na asilimia 68.6 wanawake 8.574 sawa na asilimia 31.4 walijitokeza kwa ajili ya kufaanikisha, chini ya mgeni rasmi mwenyekiti wa baraza la mapinduzi ambae pia ni rais wa Zanzibar.